Advertisements

Tuesday, April 16, 2024

TCAA YAPONGEZWA USIMAMIZI THABITI SEKTA YA USAFIRI WA ANGA



Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Daniel Malanga akiwasilisha majukumu ya Mamlaka mbele ya Kamati ya Mawasiliano Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilshi Zanzibar lipotembelea Makao Makuu ya TCAA kujionea na kujifunza shughuli za usimamizi wa sekta ya usafiri wa anga nchini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilshi Zanzibar Yahya Rashid Abdallah akizungumza mara baada ya kamati hiyo kupata taarifa ya kazi zinazofanywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Baadhi ya wanakamati ya Mawasiliano Ardhi na Nishati ya Baraza la Wawakilshi Zanzibar  wakiuliza maswali mara baada ya kupata maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) walipotembelea makao makuu wa Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.

DKT. TULIA AKIFUNGUA KIKAO CHA MABADILIKO YA TABIANCHI




Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akifungua kikao cha kujadili changamoto za mabadiliko ya tabianchi yanayoikumba Dunia na utatuzi wake, wakati wa Mkutano wa Mwaka 2024 wa Jukwaa la Kibunge la Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani unaofanyika katika Makao Makuu ya Benki ya Dunia, Washington DC, nchini Marekani leo tarehe 16 Aprili, 2024.



PICHA NA OFISI YA BUNGE

DKT. KIKWETE ATEMBELEA CHUO CHA UONGOZI CHA JULIUS NYERERE KILICHOPO NDANI YA CHUO KIKUU CHJA MAKERERE JIJINI KAMPALA, UGANDA



Rais Mstaafu Dkt. Kikwete akiwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Uongozi cha Julius Nyerere, Dkt. Nansozi Muwanga alipotembelea Kituo hicho kilichopo ndani ya Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda, jana Jumatatu.

Kituo hicho, kinachotoa mafunzo ya uongozi na kuandaa vijana kuwa viongozi bora, kinaratibiwa na chuo Kikuu cha hicho kikongwe Afrika Mashariki.

Dkt Kikwete alitembelea chuoni hapo alipoalikwa kama mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa kwanza wa marais na viongozi wa sasa na wa zamani wa serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu vya Uganda ambapo alialikwa kama mgeni rasmi. Mkutano huo, uliojadili umuhimu na nafasi ya viongozi waliopo madarakani kuandaa viongozi wanaochipukia, ulihudhuriwa na zaidi ya marais na viongozi wa sasa na waliowahi kuwa viongozi wa serikali za wanafunzi wa vyuo vikuu vya nchini Uganda zaidi ya 1,000.

RAIS SAMIA ASHIRIKI MSIBA WA MZEE MUSSA ABDULRAHMAN, UNGUJA ZANZIBAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole na kumfariji Bi. Mwanakheri Mussa Yussuf, Mjane wa Marehemu Mzee Mussa Abdulrahman ambaye alikuwa rafiki wa familia na Jirani wa karibu aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo mtaa wa Mombasa, Zanzibar. Rais Samia alifika kutoa pole msibani Kwahani Mchangamwingi Zanzibar tarehe 16 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji Bi. Mwanakheri Mussa Yussuf, Mjane wa Marehemu Mzee Mussa Abdulrahman ambaye alikuwa rafiki wa familia na Jirani wa karibu aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo mtaa wa Mombasa, Zanzibar, kushoto ni Mtoto wa Marehemu Bi. Fatma Mussa Abdulrahman. Rais Samia alifika kutoa pole msibani Kwahani Mchangamwingi Zanzibar tarehe 16 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiomba dua pamoja na Wanafamilia wa Marehemu Mzee Mussa Abdulrahman aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo mtaa wa Mombasa, Zanzibar. Rais Samia alifika kutoa pole msibani Kwahani Mchangamwingi Zanzibar tarehe 16 Aprili, 2024.

MILIONI 100 KUTUMIKA KUONGEZA MAJENGO ZAHANATI YA MADOPE,LUDEWA

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Dkt Festo Dugange amesema katika mwaka wa fedha 2025/26 Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa itatenga Sh Milioni 100 kwa ajili ya kuongeza majengo na kuanza utaratibu wa kupandisha hadhi zahanati ya Madope kuwa kituo cha afya.

Mhe Dkt Dugange ametoa kauli hiyo leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Ludewa, Mhe Joseph Kamonga aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kupandisha hadhi Zahanati za Madope na Ludewa kuwa vituo vya afya.

“ Zahanati za Madope na Ludende ni Zahanati zilizopo kwenye Makao Makuu ya Kata za Madope na Ludende Mtawalia. Zahanati ya Madope ina eneo la takribani ekari 10 pamoja na vigezo vingine inakidhi kuwa na kituo cha afya.

Katika mwaka wa fedha 2025/26 serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo itatenga Sh Milioni 100 kwa ajili ya kuongeza majengo na kuanza utaratibu wa kuipandisha hadhi kuwa kitio cha afya,” Amesema Mhe Dkt Dugange.

TAMISEMI, WIZARA YA ELIMU KUWAKWAMUA WANAFUNZI WALIOKWAMA NA MAFURIKO

KUTOKANA na hali ya mafuriko yanayoendelea, Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia zimekubaliana namna ya kuwasaidia wanafunzi waliokwa kuendelea na masomo ili waendelee na masomo.
Akizungumza leo mara baada ya kikoa kilichowakutanisha mawaziri na walaamu wa wizara hizo mbili, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mohamed Nchengerwa amesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kuna baadhi ya wanafunzi wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto ya mafuriko.
“Kutokana na hali ya mfuriko yanayoendelea nchini, mimi na mwenzangu wa wizara ya elimu (Profesa Adolf Mkenda) tumekubaliana sasa tunakazi ya kuja na mpango wa muda mfupi na muda mrefu ambao utawawezesha vijana wetu wanaosoma shule mbalimbali ambao leo hii wamekwama kuendela na masomo kwasababu ya majanga ya mafuriki yanayoendelea kote nchini hususani katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Katavi na mikoa ya kaskazini na kusini.”

Amesema katika kutekeleza hilo wizara zimewaelekeza wataalamu kutoka wizara hizo kwenda nchi nzima kufanya tathimini na kujiridhisha kutokana na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya shule uliochangiwa na mafuruki.

KINANA AKEMEA UKABILA,ASHAURI VIONGOZI WACHAGULIWE KWA SIFA

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana amekemea tabia ya baadhi ya wanaCCM na wananchi kuendekeza ukabila na kwamba ukabila ni jambo ambalo limepitwa na wakati na halina tija katika Taifa.

Amesisitiza hakuna faida yeyote ambayo inapatikana kwa kuendekeza ukabila zaidi ya kuleta mgawanyiko katika Taifa huku akifafanua Hayati Baba wa Taifa Mwalim Julius Nyerere alikemea ukabila.

“Kuwa na makabila ni jambo la kawaida ila ukabila ni jambo baya na kwamba kumuhukumu mtu kwa jambo ambalo hana uwezo nalo sio sahihi.”
Kinana aliyekuwa akizungumza na wanachama wa CCM Wilaya ya Rorya mkoani Mara moja ya malalamiko aliyopewa ni kuwepo kwa ukabila ka baadhi ya wanaCCM katika wilaya hiyo.

Hivyo wakati anazungumzia malalamiko hayo Makamu Mwenyekiti Kinana ameeleza Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alitoka katika kabila dogo mkoani hapa lakini aliongoza nchi kwa miaka 24, alipendwa, aliheshimiwa, alithaminiwa si kwa sababu ya ukabila bali kutokana na kazi nzuri aliyoitenda kwa uadilifu na kuheshimika Tanzania, Afrika na duniani kote.

WAHITIMU WA MASOMO YA SHERIA NCHINI WASISITIZWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUJISOMEA


Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma, akizungumza wakati akiongoza maadhimisho ya Siku ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) yaliyofanyika Leo Aprili 15,2024 jijini Dodoma.
Makamu Mkuu wa Chuo cha UDOM Prof. Lughano Kusiluka akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) yaliyofanyika Leo Aprili 15,2024 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (hayupo pichani), wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) yaliyofanyika Leo Aprili 15,2024 jijini Dodoma.

Na Gideon Gregory, Dodoma.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma amewasisitiza wanafunzi wanaohitimu masomo ya Sheria nchini kuwa na utamaduni wa kujisomea kwani kwasasa dunia inapitia mabadiliko makubwa ya matumizi ya Teknolojia kwenye utendaji wa kazi.

Jaji Mkuu ameyasema hayo Aprili 15,2024 Jijini Dodoma wakati akiongoza maadhimisho ya Siku ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo yameongozwa na kauli mbiu isemayo “Uimarishwaji wa kliniki za sheria vyuo vikuu katika kukuza na kupanua wigo wa upatikanaji wa haki Tanzania”.

Monday, April 15, 2024

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KONGAMANO LA KUHAMASISHA UWEKEZAJI BUSTANI ZA KIJANI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa na viongozi mbalimbali katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gaspar mkoani Dodoma alipowasili kwaajili ya kufungua Kongamano la Kuhamasisha Uwekezaji katika Bustani za Kijani Nchini kwa Maendeleo Endelevu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifuatilia mawasilisho mbalimbali wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kuhamasisha Uwekezaji katika Bustani za Kijani Nchini kwa Maendeleo Endelevu linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gaspar mkoani Dodoma tarehe 15 Aprili 2024. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Bw. Kadari Singo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Kuhamasisha Uwekezaji katika Bustani za Kijani Nchini kwa Maendeleo Endelevu linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gaspar mkoani Dodoma

RAIS SAMIA ATEMBELEA MAJIRANI ZAKE MTAA WA MOMBASA UNGUJA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na majirani zake wa zamani Bi Asha Salum Abdallah ambaye walisoma wote Shule ya Msingi na Sekondari na mume wake Inspekta Mstaafu wa Jeshi la Polisi Rashid Zam Ali pamoja na Binti yao na mjukuu alipotembelea mtaa wa Mombasa, Unguja Zanzibar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na majirani zake wa zamani Bi Asha Salum Abdallah ambaye walisoma wote Shule ya Msingi na Sekondari na mume wake Inspekta Mstaafu wa Jeshi la Polisi Rashid Zam Ali pamoja na Binti yao na mjukuu alipotembelea majirani zake wa zamani mtaa wa Mombasa, Unguja Zanzibar, tarehe 15 Aprili, 2024.

SHILINGI BILIONI 743 ZATOLEWA KWA WANUFAIKA MILIONI 6 - WAZIRI MKUU


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema katika mwaka 2023/2024, shilingi bilioni 743.7 zimetolewa kwa wanufaika zaidi ya milioni sita kupitia mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Ameyasema hayo leo jioni (Jumatatu, Aprili 15, 2024) Bungeni, jijini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuhitimisha mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2024/2025.

“Serikali imeendelea kutekeleza sera mbalimbali za uwezeshaji wa makundi maalum ya wanawake, vijana na wenye ulemavu. Lengo likiwa ni kuhakikisha makundi haya yanashiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi hapa nchini.”

Amesema katika kutekeleza sera ya ushirikishwaji wa Watanzania kwenye miradi ya kimkakati na uwekezaji nchini, wanawake na vijana wameendelea kunufaika kupitia miradi ya kimkakati na uwekezaji ambapo katika mwaka 2023/2024, Watanzania 162,968 wamenufaika na ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

KATIBU MKUU UJENZI AZITAKA TAASISI ZOTE ZIANZE KUTUMIA MFUMO WA UFUATILIAJI NA TATHMINI.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi, Mhandisi Aisha Amour, akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakati akifungua Baraza hilo, lililofanyika Mkoani Morogoro.


Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Aisha Amour (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Baraza hilo Mkoani Morogoro.

MATUKIO KATIKA PICHA OFISI YA WAZIRI MKUU BUNGENI DODOMA MICHUZI BLOG AT MONDAY, APRIL 15, 2024 HABARI,

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Mary Maganga akutambulishwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa 15 wa Bunge, kikao cha Sita, bungeni jijini Dodoma leo tarehe 15 Aprili, 2024.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Deogratius Ndejembi (kulia) akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Boniface Simbachawene, Bungeni jijini Dodoma leo Aprili 15, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais (Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi) Zanzibar, Mhe. Hamza Hassan Juma (wa kwanza kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (wa pili kutoka kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bi. Mary Maganga pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa bungeni tarehe 15 Aprili, 2024 wakati wa Mkutano wa 15 wa Bunge kikao cha Sita unaoendelea Bungeni, jijini Dodoma.

DKT. NCHIMBI AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA SUMBAWANGA


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameagiza wakandarasi kukamilisha ujenzi Machi mwakani na kwa ubora unaotakiwa. Ujenzi wa uwanja huo utakaogharimu zaidi ya sh. Bil. 60 utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 150, 000 kwa mwaka na utarahisisha zaidi usafiri kwa wakazi na wageni.

Watu 120 wamepata ajira katika mradi huo ambapo wazawa wamekuwa 114.

Dkt. Nchimbi ametoa maagizo hayo leo Aprili 15, 2024 wakati kiwaongoza viongozi wa chama na serikali kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga kwenye ziara yake mkoani Rukwa.

Dkt. Nchimbi ambaye ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla pamoja na Katibu wa Oganaizesheni, Issa Haji Gavu ameanza ziara ya kikazi ya siku kumi katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma.

MVUA ZALETA ATHARI KAVUU


Mbunge wa jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akiangalia athari ya mafiruko katika mto Kibaoni katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi.
Wananchi wakisaidia kulisukuma gari la abiria lililokwama kitokana na atahari za mafuriko katika halmashauri ya Mpimbwe mkoa wa Katavi.
Mkuu wa wilaya ya Mlele Alhaji Majid Mwanga akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maeneo yaliyoathiriwa na mvua. Wa pili kushoto ni Mbunge wa jimbo la Kavuu na Waziri wa Ardhi Mhe. Geophrey Pinda
Mkuu wa wilaya ya Mlele Alhaji Majid Mwanga akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maeneo yaliyoathiriwa na mvua. kushoto ni Mbunge wa jimbo la Kavuu na Waziri wa Ardhi Mhe. Geophrey Pinda na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mlele Wolfgun Mizengo Pinda.

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU ARIDHISHWA NA MRADI WA MAJI WA TANGA UWASA


KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 Godfrey Mnzava katikati akifungua koki ya maji baada ya kuzindua mradi wa maji wa kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Kata ya Chongoleani Jijini Tanga unaofanywa na mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) kulia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya kushoto ni Mhandisi wa Miradi wa Tanga Uwasa Mhandisi Violeth Kazumba.

Na Oscar Assenga,TANGA.
KIONGOZI wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Mnzava ameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Kata ya Chongoleani Jijini Tanga unaofanywa na mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa).

Mradi huo pia utahusisha kata za Mabokweni na Mzizima Jijini Tanga zenye mitaa 10 na wakazi wapatao 26,071 ambapo miundombinu inayojengwa katika mradi huo inakusudia kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma kwa wakazi wa maeneo hayo na hivyo kupata maji kwa kila siku kwa saa 24.

Lakini pia ikiwagusa watumiaji wengine ikiwemo wa viwanda,biashara pamoja na kampuni inayohusika na ulazaji wa bomba ka mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Jijini Tanga nchini Tanzania.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo na kuuzindua ,Mnzava alisema wameridhishwa na mradi huo wa Tanga Uwasa kutokana na kwamba wao wamekuwa wakitekeleza maelekezo ya Serikali ya kutangaza miradi yote na zabuni kwenye mfumo wa kidigitali wa zabuni (NEST).

DC SAME AMEWATAKA WANANCHI KUHAKIKISHA WANAITUNZA MIRADI AMBAYO IMEZINDULIWA NA MBIO MWENGE 2024


Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Mhe. Kasilda Mgeni (kushoto), akipokea Mwenge wa Uhuru, Kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Mhe. Abdallah Mwaipaya wakati Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024, zilipoingia wilayani kwake.


NA ASHRACK MIRAJI, SAME
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro, Mhe. Kasilda Mgeni, amewataka wananchi kuhakikisha kila mmoja kwenye eneo lake anashiriki kikamirifu kuilinda na kuitunza miradi yote iliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru 2024.

Ameyasema hayo wakati anapokea Mwenge wa Uhuru Wilayani, ambapo miradi kadhaa ya maendeleo imezinduliwa.

Amesema kwa kufanya hivyomiradi hiyo itaendelea kuleta manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo kama ilivyokusudiwa katika utekelezaji wake.

Katika Wilaya ya Same, Mmbio za Mwenge wa Uhuru 2024 zimezindua miradi nane ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3.6.