Advertisements

Monday, November 24, 2014

Video ya Binti wa Kazi "Beki 3" akimtesa mtoto

Hii Video imeenea sana kwenye mitandao ya jamii  huyu mfanyakazi wa ndani alivyomtesa malaika wa watu inasemekean hii ni Uganda pia kuna habari kwamba binti huyu wa kazi yupo mahabusu kwa mashataka ya kutaka kuua kwa makusudi. Kilichomsaidia mzazi wa mtoto huyu ni kufunga kamera ndani ya nyumba ambayo msichana wakai alikuwa hajui na vitu kama hivi hutokea sana hata Tanzania na wakati mwingine mzazi utarudi toka kazini unakuta mtoto amevimba mfanyakazi wa ndani atakuambia alinguka wakati nilipokua nasafisha jiko lakini kwa sababu hakuna kamera na tabia nzuri ya msichana wa kazi anayoonyesha nyuma ya pazia mzazi humuamini. Kitendo hiki kama mzazi ingekua mwanao amefanyiwa hivi ungefanya nini una fikiri ni sababu gani zilizomfanya msichana wa kazi kuwa mnyama kiasi hik?

4 comments:

Anonymous said...

balaa hii kitu duuuuuuuuuuuuuuu..tuwe wangalifu tunapowaacha watoto zetu na walezi.na tuwe tuna wa treat vizuri hawa walezi wetu tusipo wa treat vizuri matokeo yake ndo haya wanakuja kuwatesa watoto wetu kwa hasiri tulivyowanyanyasa wao.
yani mtu unakosa huruma na motto mdogo hivi hata kama hujaza na si wako jamani eeeeh

Anonymous said...

ndo maana wakina mama wanatakiwa wakae nyumbani kuwalea watoto wao sio eti kuwa kazini.mlee mtoto wako mpaka afeke umri wa kwenda shule ndo unaweza kurudi kazini. beside kazi za ndani ni za mama mtoto baba amsaidiye pia na kazi za baba offisini aleta pesa atunze familia yake mama abaki home alee familia.

mkibisha matokeo yake ndo haya.

inatia uchungu sana yaani wee achaa tuuuuu

Anonymous said...

na ndo maana akina baba wanatakiwa wajitume ili wawa-take care akina. ila wababa wa siku hizi wanataka mgawane bills na majukuu nusu kwa nusu sasa hapo mama kuna kukaa ndani kweli!....men of these days and ages are useless hawatakiwi hata kuitwa "kichwa cha familia". unapoamua kuoa ni kwamba tegemea kulipia pango lote la nyumba, ada za shule za watoto, lishe ya familia nk nk

Anonymous said...

mmh..hapa sio issue ya kunyanyaswa au kuwa treated vibaya.ukinyanyaswa mtu mzima kama huyu si unaaga vizuri na kwa usalama unatafuta ustaarabu mwingine?siwatetei kabisa hawa wasichana.ni hulka tu ya mtu na labda malezi aliyopata kwao.Wababa kutafuta kwa ajili ya familia walishasahau,hebu mbadilike ili tulee watoto ipasavyo.Naamini si huyo tu,hata wa kwetu ambao wameshakuwa wakubwa walionja joto hilo...hii yote ni umaskini tu.kama kuna pato la kutosha unalea hata miaka miwili..Mungu atusimamie