Advertisements

Monday, June 29, 2015

KIZAA ZAA BAGAMOYO ALIYEDHANIWA MAITI APUMUA WAKATI AKIKOSHWA!

Hospitali ya wilaya Bagamoyo ilithibitisha kuwa mgonjwa ni mauti !

Jasho lilianza kumtoka na joto kali la mwili ! Maziko hakuna tena !
Bagamoyo,
Maajabu ya mwenyezi Mungu yametokea msibani huko mjini Bagamoyo katika eneo lijukanalo kama Majani Mapana jana baada ya mwanamama moja aletambulika kwa jina Bi.Hatujuani kuthibitishwa kuwa umauti umekuta au amekufa hatimaye amepumua wakati wakimkosha na kwa matayarisho ya kuvikwa sanda ambayo tayari ilikwisha shonwa,
Bi.Hatujuani aliugua kwa muda na kukimbizwa hosptilai ya wilaya Bagamoyo baadaye kumpata sijui tuite umauti wa muda mfupi au kupoteza fahamu ! lakini hospitalini hapo walithibitisha kuwa keshakufa, mkasa huo ulitokea tarehe 28.juni 2015 na wanandugu walishachukua maiti na matayarisho ya maziko yakiwa mbioni ,Turubai lilishafungwa,sanda tayari hadi siku 29 juni 2015 wakimkosha maiti Bi.Hatujuani aka hatu mwenye umri wa miaka 30 ,waliokuwa wakimkosha walishtuka maiti kuwa anajoto kali,anatoka jasho na anakunja na kukunjua mikono na miguu ! lakini kusema wala kusimama hawezi !
Wanandugu waingia tafrani Msiba hakuna tena ! Turubai limeshaezuliwa !
baada ya wanandugu kutangazia umma kuwa msiba hakuna tena bali tuna mgonjwa maututi
waliofika msibani na umati wa watu wagoma kuondoka mazikoni hadi kieleweke nini? kilichozua mtihani huu tena katika mwezi huu mtukufu wa
Ramadhani
Hivi unavyosoma habari na turubai limeshaezuliwa hakuna msiba

6 comments:

Anonymous said...

Watu wengine wapo cheap kweli....sasa mnakataa kuondoka kwa nini? Okay mnasubiri pilau, kwani lazima mle msibani? Watanzania tuna shida ya kufanya kazi kwa kuzingatia professional, inaonekana watanzania wengi wanazikwa wazima, hakuna cha coma wala nini....mtu akipoteza fahamu au moyo ukisimama kwa dakika au mtu akikosa pumzi basi hao tayari wanamkimbiza mortuary. Waislaam ndiyo wanaoongoza kwa kuzika watu wazima.

Unknown said...

wewe mtoa hoja hapo juu unauthiditisho gani kutaja waislamu usitaje dini za watu hovyo hovyo ondoa maneno yako, na watu kusubiri siyo ktka pilau ww unaonekana uwezo wako ni mdogo wa kufikiri

Anonymous said...

Uwezo wangu wa kufikiri ni mkubwa sana pengine mara 1000 ya uwezo wako. Ndiyo maana nimetoa mawazo yangu kwenye hili tukio....sasa wewe badala ya kutoa mawazo unanishambulia. Huoni unapoteza muda wako kwa kuanza kupambana na watoa maoni badala ya kutoa comments kwenye hili lililoandikwa.....ulitegemea utanibadilisha kwa kutukana? Ndiyo maana nasema una tatizo.

Anonymous said...

Kutokana na ukweli kuwa madaktari wengi hufanyakazi kwa mazoea, hivyo kurush ku declare death ,watu wengi huzikwa wakiwa hai only that their heart rates inakuwa way below normal.

Anonymous said...

Tatizo sio waislam kuongoza kama mtoa hoja wa mwanzo anavyofiri, bali ni uwezo wa huyo (hao) daktari(madaktari) waliothibitisha hicho kifo, ndio wa kulaumiwa, ikiwa mgonjwa kapelekwa hospitali na mganga kathibitisha kuwa ana ugonjwa fulani na kumbe ni mzima hata akiwa mkiristo hana kosa na wala jamaa zake hawana kosa kwani wao sio wajuzi wa taluma hiyo.

Anonymous said...

wagalatia katika ubora wao utawaona tu;kwa misifa na kujifanya wasomi kumbe pumba tu.sasa roho yako imekosheka safi safin kwa kutaja waislamu ndo wamekukaa na roho.
ugalatia umekuziba macho hata kufikiri na kutoa madaa katika umma unakushindwa.panya kasoro macho;yako yako ya kurembuka tu.

mgalatia katika ubora wake ndo huo hapo juu.fikra finyuuuuuuuuuuuuu.finyuuuuuuuuuuuuuuu.