Advertisements

Tuesday, July 28, 2015

HATIMAYE EDWARD LOWASSA AJIUNGA RASMI CHADEMA NA AKABIDHIWA KADI

Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho,Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa leo katika hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.Picha na Ahmad Michuzi wa Michuzi Media
 Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akizungumza na mamia wakati wa kutangaza adhima yake ya kujiunga na Chadema katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

 Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya kujunga kwake katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
 Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa (mwenye umvi) akiwa na viongozi wa UKAWA katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimpa kadi ya uanachama Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Regina Lowassa leo katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
 Mh.Lowassa akiingia kwenye Hoteli Bahari Beach  kwa ajili ya kutangaza adhima yake ya kujiunga na UKAWA. Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa ametangaza kujiunga rasmi na Umoja wa Katiba (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) .
 Mh.Edward Lowassa akiwa katika hadhara ya mamia kujibu maswali katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
 Mh.Lowassa akiwa na viongozi wa UKAWA  katika Hoteli ya Bahari Beach Hoteli jijini Dar es Salaam jioni ya leo mara baada ya kutangaza rasmi azma yake ya kujiunga na ukawa.
 Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika Hoteli ya Bahari Beach Jijini Dar es Salaam jioni hii alipokuwa akitangaza azma yake ya kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA.
Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba  katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

10 comments:

Unknown said...

Ndugu mheshimiwa Lowasa,
Hongera sana sana. Mimi nakupa hongera sana kwa sababu mbili.
Wewe ni mkisto, na umepoteza imani na chama CCM.
Kama wewe uliyedumu katika chama CCM umepoteza imani ni lazima una misingi iliyokufanya upoteze imani.
Ni kweli kuwa wewe una upendo na nchi Tanzania. Upendo katika moyo
wako na kwa imani yako kama makisto kama alivyokuwa Baba wa taifa Mwalimu Nyere. Usitazame nyuma tena.
Congratulations and welcome to Chadema.
Watu wote wa mkoa wa Arusha na Manyara tumefurahia maamuzi yako.
It feels good to be accepted and to be part of family Chadema ni kama family katika mikoa hii miwili.
Mimi niko nje naishi nje lakini nasaidia sana watu katika hii mikoa miwili hasa wakina mama na watoto specifically school age children.
I will follow with this. Keep in touch.

Anonymous said...

Hongera Lowassa, kukaa CCM hakutakusaidia kitu mzee. Kule CCM hakuna haki ni uonevu tu.....hao marais wastaafu waliokukata jina wao wenyewe ni chanzo cha matatizo katika nchi yetu....kwa ufupi tu siyo wasafi hata mmoja, wengine waliuza viwanda kwa bei ya kutupa na kujimilikisha mali ya taifa letu, wengine waliharibu uchumi wa nchi yetu na kuruhusu watu Fulani Fulani waibe na waumiliki uchumi wetu kama zawadi, wengine walijichukulia viwanja na mashamba wao na familia zao, wengine hadi leo wanaendelea kuharibu uchumi wetu na kuwapendelea ndugu zao licha ya kuendelea kuiba mali yetu.Wao wanachoona ni Richmond tu kama vile wewe ndiye uliyekuwa rais mwenye maamuzi ya mwisho, wamesahau walichofanya wao....wamesahau fedha walizosema walitoa kusaidia mdororo wa uchumi kiasi cha trilioni 2.1, wamesahau EPA, ESCROW, MEREMETA, RADAR, NDEGE YA RAIS, VIFAA VYA JESHI VILIVYONUNULIWA KWA KUPAISHWA BEI NA WAHINDI, CHAVDA NA MASHAMBA YA MKONGE, UBINAFSISHAJI WA MABENKI NA VIWANDA KWA BEI YA KUTUPA AMBAVYO VINGINE VIMESHAKUWA GODOWNS, KUUZA NYUMBA ZA SERIKALI KWA BEI YA KUTUPA (NASIKIA WANAJENGA NYINGINE- WATAZIUZA TENA)

Anonymous said...

SLAA YUKO WAPI?

Anonymous said...

CCM hoiiiiiii!!! Karibu ukawa tuwazike ccm. Tumechoka dhuluma na wizi wao. Walikuchafua tu bure mkuu.

Anonymous said...

Tanzania ilihitaji mabadiliko. Na kwa kuwa hayakuwezekana ndani ya zulia la kijani basi ieleweke wazinkuwa yanaweza kupatikana nje. Lowassa ni vyema aachwe alikotaka kwenda na bora asifuatwe kwani ni kuleta mvurugano ndani ya nchi yetu wenyewe. Tusonge mbele waTanzania wanahitaji kuishi kwa amani. wanahitaji kuishi kwa amani. Mrema alianza mwachieni Lowassa amalize.

Anonymous said...

Hongera mh. Lowassa ni uamuzi mgumu sana.Mungu akusimamie. Pia mama Regina uwe shupavu kwa wakati huu mgumu

Anonymous said...

Kwa nini Daktari Slaa anang'atuka kiti chake; yaani, kwa nini alisimama na kuondoka kiti alichokuwa amekalia hapo pichani?

Unknown said...

Nukuu za baba wa taifa la Tanzania. Nasema tena nukuu au masisitizo na wasaa wa baba wa Taifa la Tanzania nafikiria zilikuwa nasaa zake za mwisho mwisho kabla hajaaga hii dunia . Ni kwamba ukimuona mtu anahangaika kwa mamma yeyote kuingia ikulu huyo mtu ni wa kuogopwa kama ukoma. Ukoma ni maradhi yaliowahi kutikisa dunia kiasi kwamba watu waliowahi kuathirika na maradhi hayo ilibidi wajengewe makazi yao mbali kabisa na jamii kwa kifupi kiboko kuliko ukimwi kwa sababu unaweza kuishi makazi mamoja na muathirika wa ukwimi lakini ukoma huthubutu mpaka sasa nikiboko juuu ya magonjwa balaa. Sasa bila ya kumumunya midomo yetu mwalimu nyerere anatuambia Lowasa ni mtu wa kuogopwa kama ukoma. Hao wanaosema hongera lowasa ni wasaliti wa mwalimu na ni wasaliti wa haki wenye nia ya kuiyabudu rushwa na ni wasaliti wa wawatanzania. Wanahahangaika jinsi ya kuwadanganya watanzania kuwa lowasa sio tatizo bali tatizo ni ccm. Matatizo ya ccm yanasababishwa na watu kama kina lowasa sasa leo hao wanaojiita watu makini katika kuwaletea watanzania utawala bora na as haki wanamuona lowasa ni mtu sahii kuiongoza nchi hii ingali bado inamadonda mabichi ya ya rushwa na upotevu wa mamilioni ya pesa kwa kweli inakera. Dk slaa angeleta upizani wa kweli mbele ya ccm katika uchaguzi unaokuja sio lowasa no doubt bout that kama kweli hawa watu wangekuwa makini kama ambavyo wanavyowadanganya watazaniwa. Chadema na ukawa wenu mmetusaliti watanzania lakini tutawajibu vilivyo kwenye uchaguzi mkuu.

Anonymous said...

Kwanini CCM wameumizwa sana na Lowassa kuhama chama? Mi nilidhani wangefurahia kama CHADEMA walivyofurahia kuondoka kwa ZZK. Kama mtu hamumpendi ndani ya chama anapoondoka mnatakiwa mfurahi. Sasa kwanini CCM wameumizwa na kupata hofu ya ghafla?
Jana kamati kuu ya CCM imekutana kwa dharura kujadili suala hili. Mzee Kingunge amedhibitisha pia kuwa Rais Kikwete jana akiwa Australia amempigia simu Eddo mara 18 bila Eddo kupokea. Swali; kwanini CCM wanahangaika? Kwanini wanapata pressure kwa mtu waliyemkataa?
CCM wanadai Eddo ni mchafu, lakini wanaumia yeye kuondoka. Hivi unaumiaje mtu mchafu kuondoka? Mi nadhani kama mkeo ni mzinzi, mchawi, mhuni etc, anapoondoka unatakiwa ufurahi sio usikitike. Sasa wenzetu wamesikitika hadi wameshindwa kuficha. Yani inawauma mno. Kwanini?

Unknown said...

Oscar
Kila jambo zuri wenye hila hawalipendi Lowasa jembe la mabadiliko umefika wakati muafaka wa CCM Kuacha kuishi ndani ya chama kwa mazoea kama vile chama
ni cha kichifu.Huo ndio ukomavu wa kisiasa,Onyesha uwezo wako kutetea maslahi
ya nchi yaliyoporwa na wachache wenye uchu wa madaraka ili kulinda uovu wao.TUTAKUPA KURA ZOTE WENYE HILA WAJUTE.