Advertisements

Wednesday, September 30, 2015

‘Toroka Uje Ya Ukawa’ Kusomba Vigogo Hawa Wa CCM..? HII BALAA SASA


Taarifa tulizozipata zinaeleza kuwa Kambi ya Ukawa imepanga kuzindua rasmi kampeni yake walioyoipa jina la ‘Toroka Uje’, ikiwa na nia ya kuhamasisha watu wengi kukitoroka Chama Cha Mapinduzi na kumuunga mkono mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa chanzo chetu, baadhi ya majina ya vigogo wa CCM wanaodhaniwa kuwa huenda wakajiunga na kambi ya upinzani kupitia kampeni hiyo ni pamoja na mwana siasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru.
Wengine wanaotajwa kuwa huenda wakajiunga na Ukawa ni pamoja na waziri asiyekuwa na wizara maalum, Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Sophia Simba na Balozi Juma Mwapachu.
Hata hivyo, Sophia Simba ambaye aliwahi kupinga wazi uamuzi wa Kamati ya Usalama na Maadili ya CCM kulikata jina la Edward Lowassa, aliwahi pia kukanusha kuwa na mpango wa kumfuata mwanasiasa huyo katika kambi ya upinzani.
Jina la Profesa Mark Mwandosya na Mzee Kingunge ni kati ya majina ya watu waliopinga waziwazi uamuzi wa CCM kulikata jina la Lowassa kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea urais, ambapo Dk. John Magufuli alichaguliwa kati ya wagombea 42.
Profesa Mark Mwandosya aliwahi kusikika akieleza kuwa wajumbe wa kamati ya Usalama na Maadili pamoja na mwenyekiti wa Kamati hiyo ya CCM walikuwa na majina yao mfukoni.
Baada ya kujitokeza hadharani kupinga uamuzi wa CCM, Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) ulimvua madaraka aliyokuwa nayo katika umoja huo kwa madai ya kutokuwa na imani naye baada ya kukiuka taratibu za chama.
Tuendelee kusubiri matokeo ya kampeni ya ‘Toroka Uje’ ya Ukawa, huku tukisubiri pia matokeo ya kampeni ya ‘Nimeshtuka’ ya CCM, zote zikiwa na lengo moja la kusomba wafuasi wa vyama. Je, nani atavuka kwenda ng’ambo ya mto? Majibu yatapatikana hivi karibuni kwani zimebaki siku 25 tu.

8 comments:

Anonymous said...

Nilisema halo halo karibuni wazee wetu
Tubadilishe mfumo na maisha ya Watanzania
Lowassa
Lowassa
Lowassa
Na
Ukawa
Ukawa
Ukawa

Anonymous said...

Ushuzi mtupu Sophia Simba yupo safarini New york city na Kikwete hata hivyo hizo propanda zisizokuwa na mshiko kwa wakati huu sawa sawa na kukumbuka shuka wakati kumeshakucha kwani Magufuli amefanikiwa kuendesha campaign za maana sana na kuwavuruga wapizani wake vibaya vibaya mpaka hapa tulipo fikia there is no way out ukawa can catch with him up kwa muda huu uliobakia kabla uchaguzi na ndio maana utaona ukawa wamekuwa wakitoa kauli za kimihemko zisikuwa na maana hizo ni dalili za kuchanganyikiwa.

Unknown said...

Anonymous 2
Unafatilia vizuri campaign au unashadadia????,!!!!

Anonymous said...

Kula Tano mdau hapo juu ukawa watasambaratika soon,,,, Bado siku 24 tuuuu,,,, tingatinga linatua Ikulu hata hao wanataka kuhama waendeee,,,, wanajijua hawana nafasi ccm tena ndio walikua kikwazo,, CCM mpooooooo,,,,,, popo bawa ukawaaaa.

Anonymous said...

KINGUNGE MWACHE AENDE KWA SABABU YEYE NDIO SABABU TANZANIA MASKINI KUPITA KIASI.HANA NAFASI KWENYE HII DIGITAL CCM.

Anonymous said...

pole sana hapo juu 2.55am mwenzetu bado kipofu...huyu Pombe analeta yale yale ..umaskini na ujinga wa mbele kwa mbele....lakini endelea kusupport things which have no progress....just compare ccm ya 1990 na ya sasa na angalia nchi inaelekea wapi kama siyo tunarudi nyuma

Anonymous said...

Ndio kazi ya Ukawa kusubiri watoro na makapi ili shughuli zao ziende..

Anonymous said...

CCM ndani ya Ikulu tena 2015. Ukawa yawa Ukiwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!