Advertisements

Saturday, November 21, 2015

VITANDA VYA MAGUFULI TAYARI MUHIMBILI

 Vitanda alivyoagiza Rais Dkt John Magufuli vikifungwa hospitali ya Muhili mapema leo baada ya Mhe. Rais kupunguza kiasi cha fedha zilizochangwa na wadhamini wa mchapalo wa Wabunge na kuagiza vinunuliwe vitanda Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alikuta wagonjwa wengi wakiwa wamelala chini siku alipofanya ziara ya kushutukiza kwenye hospitali hiyo kukagua utendaji wa kazi.
 Mafundi wakiendelea na uunganishaji wa vitanda.

15 comments:

Anonymous said...
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous said...

Haya mnaomsagia Magufuli mseme tena anakulupuka. Kuna watu hawajazoea kuona mtu mchapa kazi wakiona eti serikali si ya mtu mmoja. Wengine hatujali ni ya mtu mmoja au maelfu tunachotaka matokeo. Tulikuwa na serikali ya maelfu kazi yao ilikuwa kupanda ndege na kuoa wake wadogo hio biashara imekwisha. #Hapakazitu

Anonymous said...

Mungu akubariki Mh Raisi

Anonymous said...

Nikiskia na kuona matendo ya Magufuli kali kama tulikuwa hatuna serikali kabla yake. Anawapa somo kali kaka zake waliomtangulia kuwa kiongozi wa nchi maana na kazi yake nini

Anonymous said...

Vishaitwa vitanda vya Magufuli! Hebu tuheshimu lugha sadifu.! Ni vyema wizara husika ikatambua kuwa vitanda vinatakiwa kuwa vya aina tofauti kukidhi mahitaji hata ya kumhamisha mgonjwa akiwa kitandani (patient transferable bed)! Hata kama gharama iko juu. Isije kuwa kazi hii imekuwa rahisi na kumbe ni mradinwa mmoja wa wakwepa kodi. Hii michango kumbe inawezekana kuboresha hata maeneo mengine kwani zimechangwa na wenye uwezo, makampuni na benki!! Kwa sherehe ya wabunge!! Kumbe nao wanaweza kichanga kujenga na kuboresha miundo mbinu ya vijijini! Asante mh. Rais JPM. Hapo.utakuta kuna wakwepa kodi pia wamechanga sana!! Kaza uzi usiyumbishwe.

Anonymous said...

Kitanda ni moja, mbili ni vifaa vya tiba kama CT-Scan, MRI, X-ray n.k, tatu ni madaktari, wauguuzi na wataalamu wa kusoma hivyo vipimo wenye ujuzi na nidhamu na wenye kuwajali wagonjwa wote, nne kuwe na madawa ya kutosha, tano utaratibu wa kuwapatia bima ya afya watanzania wote (Rwanda asilimia 95 wana bima ya afya yenye kueleweka na asilimia 5 wanasaidiwa bima bure na serikali). Vitanda pekee havitoshi na havina maana bila ya kuwa na vyote nilivyotaja kwani wagonjwa hawaendi Muhimbili kulala bali kutafuta huduma bora. Huduma hizo zote zifanyike hospitali zote za mikoa na wilaya ili watanzania wote wapate hizo huduma kwani kila mwananchi ana haki ya kupata huduma bora za matibabu na kila mmoja wetu ana haki ya kuishi, siyo wananchi wa Dar eS Salaam tu pekee.

Anonymous said...

WaTZ mpaka Rais asema ndiyo kitu kifanyike kwanini wabunge hawakuliona hili mapema. nakuombea Mh. JPM Mungu akuzidishie na akulinde. kila ukifungua mdomo wako kitu chema kinatokea ambacho hakikuwezekana kabla.

Anonymous said...

Nyie ccm acheni zenu. Everything here's been cooked. Stories of this president since day one sounds like a prepared or cooked story telling. It's not real. Kama ni kweli, kama hivyo vitanda na magodoro na kila kitu huwa vipo kwa nini wasipewe wagonjwa hapo nyuma kuliko kuachwa walale chini. So within a day or two kila kitu kikapatikana. Even my three year old son can figure this mazingaumbwe out. Nyie ccm acheni kuwalaghai na kuwadanganya wananchi. At the same time, kumbe hela zipo za kuwatunza wananchi huh! Watu wanaweza kuchanga zaidi ya Sh million 250 in less than a day za kutanua na sherehe lakini hawawezi kuchanga millions kwa ajili ya kuwasaidia wananchi. Something is wrong here.... ccm oyeee!!!

Anonymous said...

kimoja bei gani,inawezekana kabisa,na nina imani ndivyo ilivvyo idara ya manunuzi imejipatia mradi wa kujinufaisha.kitanda kimoja kama hki parlay keko ni shilling 50,000.kwa hali hiyo kwa million 200 ilitakiwa vinunuliwe vitanda alfu nne [4000],na visambazwe tanzania nzima sio muhimbili tuu,shida ipo kila mahali.sasa ndipo utakapoanza kugundua kuwa kikwete alikua ni kiongozi wa aina ipi.huu ni mwanzo tuu.

Anonymous said...

Jamani hivi vitanda havifai kuwa vya hosp...sasa mgonjwa akitakiwa kuhamishwa inakuwaje...mbona vinaonekana local local sana ...mmmhhh sijui tutafika lini

Anonymous said...

Watanzania tumekuwa hatuna shukrani kama sehemu ya kutolea haja kubwa maana hata paoshwe vipi bado harufu yake haipendezeshi. Wagonjwa walikuwa wanalala chini hospitalini hata katika picha za Dk Magufuli alipotembelea pale hospitalini tulijionea kwa macho yetu wangonjwa wakimsalimia mueshimiwa raisi wakiwa wamekaa au kulala chini kabisa. Leo hii mueshimiwa raisi anapambana kuiondoa ile hali na kuwaondoshea adha wagonjwa watu wanaanza kuleta siasa. Eti ooh CCM everything concerned mr president has been cooked? How bout being your rotten mind been cooked before thinking about some one else? Mwngine aah bei gani ? Ni upuuzi mtupu. Hao walio nunua hivyo vitanda wanajua kabisa kwamba ipo siku Magufuli atakwenda kuvikagua hivyo vitanda vina ubora gani. Au hujasikia kwamba Dk Magufuli alisha muamuru mjenzi wa bara bara aifumuwe yote kwa kosa ubora. Ndio Dk Magufuli ni mzee wa viwango sahihi ni msomi na mkemia wa kiwango cha PHD. Watu wa dini wanasema Mungu anamchukia na kumuadhiri mtu ambae hukaa na kusubiri mtu fulani afanye makosa ili yeye apate cha kusema . No one is perfect na Mr Magufuli kama binaadamu yeyote hayupo perfect na hatakuwa perfect kwa sababu M/mungu peke yake ndio yupo perfect . Lakini kutokana na moyo wa imani na uadilifu alionao Dk Magufuli katika kutimiza wajibu wake basi M/mungu anamsaidia katika kufanya vitu ambavyo vinawaduwaza watu wengi sana hadi kushindwa kuamini masikio na macho yao nini kinaendelea lakini huo ndio ukweli yakwamba jamaa hata hajaanza kazi basi kazi zishaanza kufanyika sasa kama wewe unasapoti mafisadi endelea kubaki huko ila kuna Tanzania mpya ya Magufuli.

Anonymous said...

Huu ni mwanzo mzuri. Tuna hospitali nyingi na matatizo mengi. Hatuwezi kuyamaliza yote kwa mara moja lakini kama tukipunguza makali ya tatizo moja baada ya jingine, baada ya muda tutakuwa tumeendelea.
Tusilaani kwamba Muhimbili wamepata vitanda wakati hospitali za mikoani hazijapata. Tushukuru kwamba kiongozi ameenda Muhimbili kukagua, ameona matatizo na kuyafuatilia kiasi cha kuleta unafuu. Kama kila kiongozi akifanya hivyo popote alipo tutasonga mbele.
Tukumbuke kwamba sisi ni Watanzania kwanza, vyama vinakuja baadae. Tusiombee Dk. Magufuli ashindwe kazi kwa vile si mtu wa vyama tunavyovifuata maana hiyo itakuwa inamaanisha hatuna imani na vyama vyetu kufanya mambo makubwa kuliko tunayoyaona. Tumwombee afanikiwe hata kama tuna imani vyama vyetu vinaweza kufanya makubwa zaidi.

Anonymous said...

Walipokuwa wanalala chini walikuwa wanahamishwa vipi?

Anonymous said...

Inaelekea wewe bado uko kwenye kampeni za vyama,watanzania walio wengi wamekwishapita stage hiyo, hivyo vi vema uka ungana nao kujenga taifa.

Anonymous said...

AMA KWELI WASHIRIKI WENGINE KWENYE MICHANGO YA MAONI KATIKA MITANDAO YETU NI MATATIZO.NILISEMA MILLION 200 INGETOSHA VITANDA 4000 AMBAVYO VINGEWEZA KUSAMBAZWA HOSPITALI ZA SERIKALI NCHINI KOTE,NA NIKAGUSIA BEI YA KITANDA KIMOJA NA WAPI VINAPOPATIKANA.NILICHOSHUHUDIA NI MIPASHO ISIYO TIJA HASA KUTOKA KWA WANA CCM WANAOPIGANIA KUJIKWEZA KWA MHE.MAGUFULI. MATUMIZI MABAYA YA KUTISHA, NA UHUJUMU MHESHIMIWA MAGUFULI KESHAMSHIKA UCHAWI MTANGULIZI WAKE JAKAYA KIKWETE,SASA TUMSAIDIENI,TUMUOMBEE KWA MUNGU AIMARIKE AZIDISHE UJASIRI HATIMAYE IPELEKWE SHERIA MPYA YA KUFUTA KINGA YA KUSHTAKIWA KWA VIONOZI WASTAAFU BUNGENI ILI KAMA MSTAAFU ALIHARIBU AKIWA MADARAKANI BASI SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE. UKAWA KWA HILO TUTAKUWA PAMOJA NA MHE.MAGUFULI ILI KAZI YA UKWELI IWEKWE WAZI. NINAVYOONA HAKUSEMA TUU MHE.MAGUFULI KWAMBA ANAZIUNGA MKONO TAKWIMU ZA MHESHIMIWA MBATIA KWA ASILIMIA MIA MOJA-100%