Advertisements

Tuesday, May 24, 2016

HARMONIZE NA JACQUELINE WOLPER NI MAPENZI YA KWELI AU KUNA MCHEZO UNAENDELEA HAPO?

Harmonize na Jacqueline Wolper ni couple mpya town. Kwa wengi katika hatua za mwanzoni walidhani wawili hao si wapenzi bali wanatafuta tu kiki.
Lakini kadri siku zinavyoendelea kwenda, tumeshuhudia kuwa ni kweli wawili hao ni wapenzi na wanaonekana kudatishana haswaa. Kuna sababu nyingi zilizofanya watu wasiamini uwepo wa couple hiyo na kubwa zaidi likiwa ni miezi michache iliyopita Wolper alichumbiwa na mwanaume mwingine na tukaamini kuwa sasa mrembo huyo ameamua kuanzisha familia.
Hivyo baada ya kumuona akiwa na bwana mdogo Harmonize, maswali yalikuwa mengi ya kuhusu kipi kilichotokea katika uchumba wake na mwanaume huyo.
Na kwakuwa sasa tunaona kuwa wawili hao wameamua kuuweka wazi uhusiano, jibu ni kuwa Wolper na mwanaume huyo walivunja uchumba wao. Wolper anatarajiwa kuzungumza zaidi kuhusu sababu za kuachana mwanaume huyo tajiri kwenye show ya Take One ya Clouds TV leo usiku.
Sababu ya pili ni utofauti wa umri kati ya wawili hao. Harmonize ni mdogo mno kwa Wolper japo wanasema mapenzi hayaulizi kwanini na umri si kitu bali ni namba tu.

Wakati ambao kila mtu ameshathibitisha kuwa wawili hao ni wapenzi, baadhi ya watu wanadhani kuwa mapenzi yao yamekuwa na chumvi nyingi ndani ya muda mfupi na ni kama wanalazimisha watu waamini kuwa wanapendana.
Katika wiki mbili hizi, post nyingi za Wolper ni za picha yake akiwa na mpenzi wake huyo ambaye yeye amuita Raj. “Pale mahaba yanapozidi paka macho yanaanza kufanana, u have my heart Raj,” ameandika kwenye picha moja. Harmonize bado ana aibu kiaina kuanika penzi lao lakini amekuwa akitupia picha mbili tatu za Wolper anayemuita pacha wake.
Lakini wawili hao wamekuwa gumzo zaidi wiki baada ya kuhudhuria kwenye birthday ya mtoto wa Aunty Ezekiel na Mose Iyobo, Cookie aliyetimiza umri wa mwaka mmoja. Wakiwa mbele ya Diamond na wageni wengine waalikwa, hawakuonekana kutoshana kwakuwa muda mwingi walikuwa wakishikana na kubadilisha mate bila aibu.
Video inayowaonesha ‘love birds’ hao wakibadilishana mate hadharani imesambaa mtandaoni na kuzusha maswali mengi kuhusiana na jinsi wanavyoupeleka uhusiano wao. Kwa wengi wanaona kama wana show off zaidi na kwamba uhusiano wao umebeba picha ya kiki kuliko uhalisia wa watu wawili wanaopendana.
Kwenye video hiyo Diamond anaonekana kutojali kilichokuwa kikiendelea kulia kwake wakati kijana wake Harmo alikuwa akishushiana mabusu na mafrench kiss ya kumwaga na ex wa bosi wake.
“Mkwe leo mmejua kutuchafulia insta… yani kama sabuni ya unga uliyontolea watu MAPOVU,” ameandika Diamond kwenye post yake.

Hata hivyo kwa showbiz, uhusiano huo utamfaidisha zaidi Harmonize ambaye anaonekana kufuata nyayo za bosi wake kwa kuziteka headlines kwa story za uhusiano na mastaa.

1 comment:

Anonymous said...

Wewe Harmonizer huyo mwanamke siyo size yako, utamperepweta tu! Aliyekutafutia kakupoteza