Advertisements

Sunday, January 15, 2017

Miss TZ akatwa Mapanga


Na Richard Bukos, Gazeti la Risasi Toleo la Jan 14, 2017 GPL
DAR ES SALAAM: INASIKITISHA SANA! Mrembo aliyefahamika kwa jina la Queen Nazil aliyeshiriki mashindano ya Miss Tanzania 2016 akitokea Wilaya ya Ilala jijini Dar, hivi karibuni alikumbwa na janga kubwa baada ya kuvamiwa na watu waliodaiwa ni vibaka kisha kumpora vitu mbalimbali kabla ya kumjeruhi kwa mapanga, Risasi limelinyaka tukio zima.
Rafiki wa karibu wa Queen aliyeomba jina lake lisitajwe gazetini alisema kuwa, tukio hilo lilitokea usiku wa wikiendi iliyopita maeneo ya Mwenge-Mpakani jijini Dar wakati mrembo huyo akitokea kwenye mishemishe zake.

“Ilikuwa usiku wakati anatoka kwenye mambo yake, sasa aliposhuka kwenye gari ya rafiki yake kisha ile gari kuondoka, yeye alibaki getini akigonga ili afunguliwe lakini ghafla ikatokea bodaboda iliyokuwa na watu wawili ambao walimpora mkoba wake.
“Sasa kwa kuwa ule mkoba ulikuwa na simu aina ya iPhone 6, pesa shilingi laki mbili na vikorokoro vingine, Queen alijikuta akijitetea na ndipo mmoja wa wale watu alipomkata mapanga kichwani, akadondoka chini na kuanza kuvuja damu,” kilidai chanzo hicho.
Ikadaiwa kuwa, baada ya kujeruhiwa walitokea wasamaria wema ambao walimchukua mwanadada huyo aliyetajwa kuwa ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Tumaini kilichopo Mwenge jijini Dar, wakamkimbiza kwenye hospitali moja iliyopo jijini Dar kwa ajili ya matibabu.
Baada ya kuwepo kwa madai kuwa, Queen ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini tawi la Dar, waandishi wetu walifika chuoni hapo na kufanikiwa kuzungumza na Waziri wa Mawasiliano na Habari wa serikali ya wanafunzi, Grey Paul aliyekiri kumtambua na kwamba kweli alipatwa na balaa hilo.
“Ni kweli Queen ni mwanachuo wa hapa, kwa mujibu wa taarifa nilizozipata alivamiwa na watu ambao wanadaiwa ni vibaka, wakampora simu na pesa.
“Inasemekana alikuwa karibu na nyumbani kwa dada yake aliposhushwa kwenye gari ya rafiki yake na kabla hajafika getini alivamiwa na kuporwa vitu hivyo pamoja na kupigwa panga,” alisema Grey.
Hata hivyo, kiongozi huyo wa wanafunzi alisema kuwa, kwa muda huo alikuwa hajui alikokuwa akiishi Queen baada ya kutoka kwenye hosteli za chuo hicho zilizopo Mwenge.
Risasi lilifanikiwa kupata namba ya simu ya Queen lakini kila ilipokuwa ikipigwa ilikuwa haipatikani huku dada mmoja aliyedai ni rafiki yake wa karibu akisema:
“Queen ni rafiki yangu mkubwa ila siwezi kuwapeleka alipo, mwenyewe hataki hili tukio likuzwe kwani litawapa presha wazazi wake.
“Ila in short (kwa kifupi) baada ya tukio lile alipatiwa matibabu na sasa anaendelea vizuri,” alisema rafiki huyo wa Queen aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.

2 comments:

Anonymous said...

Hizi picha za nini jamani ?

Anonymous said...

Pole Queen. I hope you getter better soon. Hawa vibaka waliyofanya kitendo hicho cha kinyama kwa kumjeruhi huyu binti siku yao ya kupata majanga na balaa lazima itafika tu. What goes around comes around.