By Mwandishi Wetu, Mwananchi
Dar es Salaam. Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Augustino Mboje amesema kuwa hivi sasa wanakamilisha taratibu za kumtoa gerezani Nguza Viking na mwanaye Papii Kocha.
Mboje amesema hayo baada ya Rais John Magufuli kuwasamehe wafungwa hao ikiwa ni miaka 56 ya uhuru wa Tanzania.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi jioni, Mboje amesema sasa hivi wanajaza fomu na itakapofika saa 11 watawaachia wafungwa hao.
Tarari ndugu jamaa na marafiki wa wanamuziki hao wako nje ya gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam wakiwasubiria.
Ndugu hao ambao wameonekana wakiwa kwenye magari huku wengine wakizunguka zunguka nje ya gereza hilo kusubiria taratibu za wanamuziki hao kukamilika ili waachiwe.
Soma: Babu Seya, Papi Kocha waachiwa huru
1 comment:
Uhuru wa tanzania jamani? Uongo huu watu wazima mpaka lini.. Semwni kqeli.. Uhuru wa tangantika. Tanzanua tokea kuanziswa kwake haijafika miaka 56. Kuweni wakweli viumbe nyinyi.
Post a Comment