Advertisements

Wednesday, April 25, 2018

BINTI WA MIAKA 20 AMUUA MDOGO WAKE AMFICHA UVUNGUNI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel
By Emmanuel Mtengwa, Mwananchi emtengwa@tz.nationmedia.com

Mtoto wa miaka miwili amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali kitovuni na kuwekwa uvunguni mwa kitanda nyumbani kwao Kigamboni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula amezungumza na Mcl Digital leo Aprili, 25 na kuthibitisha tukio hilo.

Kamanda Lukula amesema kuwa tukio hilo limetokea juzi Jumatatu ambapo inadaiwa kuwa binti wa miaka (20) alimchoma mtoto huyo kwenye kitovu kwa kutumia kitu chenye ncha kali na kumficha uvunguni.

“Ni kweli tukio hilo limetokea juzi, aliyefanya hilo tukio ni binti wa miaka 20 ambaye ni ndugu wa mama wa marehemu. Si mfanyakazi wa ndani kama wengine wanavyodai, alimchoma huyo mtoto na kumlaza kifudifudi uvunguni kisha akaondoka,’’ ameeleza Kamanda Lukula na kuongeza:

“Sijapata majina sahihi maana nilielekeza niletewe na bado sijaletewa lakini tukio hilo ni la kweli.’’

Kamanda Lukula amesema baada ya huyo binti kufanya tukio hilo aliondoka nyumbani hapo.

“Huyo binti baada ya kufanya hilo tukio alikwenda kwa mwanaume anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na baada ya mama wa mtoto kurudi kazini hakumkuta nyumbani,’’amesema

Baada ya uchunguzi wa polisi, binti huyo alikamatwa na alikwenda kuwaonyesha alipomuweka mtoto uvunguni mwa kitanda.

Kamanda Lukula amesema kwa sasa taratibu nyingine za kisheria zinaendelea baada ya mtuhumiwa kukamatwa.

No comments: